Ulimwengu umeanza kuonyesha
juhudi tele za kumkomboa dinadam na
changamoto zake zinazomkabili katika maisha yake na siku ya leo tutatizama hasa
zaidi kuhusiana na kuanzishwa kwa siku ya mtoto wa afrika ikiwa ni moja ya
harakati zinazofanyika ili kumkomboa mtoto
kutoka katika unyanyasaji wa aina yoyote na mazingira magumu, anayopitia.
Siku ya mtoto wa afrika ni siku muhimu kwa watoto ambao
huazimishwa juni 16 kila mwaka huku ikiwa na lengo la kutambuaa thamani,utu na
umuhimu wa mtoto duniani .Pia siku ya mtoto wa afrika ni sehemu muhimu yenye
lengo la kutathimini masuali muhimu ya watoto hasa kupatikana kwa elimu ya
watoto wenye ulemavu, wenye vipaji maalum, yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi au magumu ili kuwapatia huduma muhimu katika maisha yao.
Siku hii kila inapoadhimishwa huambatana maandamano ya
watoto, usomaji wa risala zenye ujumbe unaohamasisha serikali kusaidia katika
masuala ya elimu pamoja na burudani mbalimbalii.
Sika ya motto wa afrika
ilianzishwa juni 16,1991 baada ya kutangazwa rasmi na jumuiya ya umoja
wa afrika ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka
1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa
shule za Soweto afrika ya kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa
inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu.
Maandamano haya yalipokelewa na
utawalwa wa kibaguzi ambapo hawakuweza kuwapatia haki zoa walizokuwa
wanazidai na mwisho wa maandamano hayo
ilikuwa ni damu kumwagika na vifo vya mamia ya wanafunzi.
Mwaka huu nchini Tanzania maadhimisho haya yameandaliwa na shirika la
planning international na wadau wengine ambapo watoto wa mitaani walikusanyika na kuandamana katikati ya jiji
la dar es salaam wakidai haki zao kwa
jumbe za maandishi.
Ukweli ni kwamba suala zima la
elimu kwa watoto pamoja na mifumo inayotumika katika elimu kwa baadhi ya nchi
imekuwa na changamoto,mfano kwa wanafunzi wengi
uwezo walionao wa kufikiri
haulingani na elimu walizopata,ama utakuta wanafunzi wangine wameacha shule kwa
sababu ya mimba na wengine changamoto za kiuchumi kwa wazazi wao kushindwa
kuwasomesha.
Mambo kama hayo sote kwa pamoja
kwa kushirikiana na serikali tunapashwa tuonyeshe nia ya dhati kwa watoto
tunaowalea na wale wa mitaani kwa malezi yanayostahili na kupigania haki zao za
msingi ili siku moja tuje kujivunia kukiona kizazi kilicholelewa katika maadili
mema…………..
Watoto wakicheza kwa furaha |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni