Kumlea mtoto maana yake ni nini ?
Ni kumtunza na kumfundisha/kumuelimisha mpaka afikie mahali pa kujitegemea mwenyewe.
Ni kumtunza na kumfundisha kwa vitendo na maneno mpaka awe mzima, kiakili na kiutu kiasi cha kuweza kuendelea mwenyewe bila ya kukutegemea.
Njia ipasayo kumlea mtoto ni ipi?
Ni njia ile nzuri yenye maadili mema yanayokubaliwa na Neno la Mungu pamoja na jamii unayoishi katikati yake.
Mwenendo wenu ni fundisho kubwa kabisa mbele ya mtoto wenu. Njia ipasayo kumlea mtoto ni kuketi na mtoto na kumshauri maadili mema ya maisha (Kumb 6:7). Ni kumwelekeza kwenye mambo matakatifu, kabla hajaharibiwa na walimwengu.
Kwa mfano:-
- Ibada za nyumbani kwa wazazi pamoja na mtoto/watoto ni kitu muhimu sana.
- Unavyowaelekeza watoto wako kuhusu maadili mazuri kwa waliomzidi umri.
- Adabu na heshima mezani mkiwa peke yenu na watoto au mbele ya wageni.
- Ikiwa wewe ni omba omba kila wakati hata watoto wako watakua hivyo.
Mzazi ni mwalimu wa kwanza kabisa kwa mtoto, Hivyo kila utakalomfundisha mwanao atalizingatia na kulishika siku zote za maisha yake.
Yale anayoyaona kwako anajifunza na kuyatendea kazi: kwa mfano,
-kusema uongo, kuahidi bila kutimiza ahadi,
kutukana nk
- Ukifanya kazi au kuishi katika hali ya uvivu usishangae mtoto wako akiwa mvivu.
- Ukiwa na bidii au ulegevu katika mambo ya Mungu, mtoto wako atakuwa hivyo.
Ukiwa na hali ya usengenyaji na kuwadharau wengine mtoto wako atayaiga hayo.
- Ukifanya kazi au kuishi katika hali ya uvivu usishangae mtoto wako akiwa mvivu.
- Ukiwa na bidii au ulegevu katika mambo ya Mungu, mtoto wako atakuwa hivyo.
Ukiwa na hali ya usengenyaji na kuwadharau wengine mtoto wako atayaiga hayo.
Kumbuka
unayomfundisha mwanao kwa vitendo, yaweza kuwa picha nzuri au mbaya ambayo
kwake itakuwa vigumu sana kuisahau au kuiacha hata atakapokuwa mzee!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni