Mtoto ni mwanadamu mwenye umri mdogo asiye mtu mzima bado. Kuna
tofauti katika tamaduni mbalimbali kuhusu umri ambao mtu si mtoto tena.
Mtoto ni Yule mwenye umri wa miaka kuanzi 0
mpaka miaka 17 mara nyingi miaka kabla umri wa 18 inatazamiwa kuwa ni kipindi
cha utoto na baadaye mtu anaitwa kijana.
Asilimia kubwa ya watoto waishio afrika
wanakosa haki zao kama watoto, na hii ni kwa sababu waafrika walio wengi ni
mwenye hali ngumu kimaisha na awana elimu ya kutosha kuhusiana na watoto.
Tunaelewa kuwa mtoto ana haki ya kusoma na wajibu wa kusikilizwa, mtoto ana haki ya kupata elimu kwa ajili ya maisha yake ya baade kwani elimu ni ufunguo wa maisha, na wajibu wa
kumsikiliza mtoto ni wa wazazi wote wawili yaani baba na mama.
Vilevile mtoto ana haki ya kuthaminiwa na
wajibu wa kuwathamini wengine, kama wazazi wakiwa wanawathamini watoto wao
na wakiwafundisha mambo mema na tabia
njema kwa kila mtu hakiki mtoto atakuwa na tabia njema.
Mtoto
ana haki ya kusikilizwa, kwa kawaida wazazi awana tabia ya kuwasikiliza
watoto wao hususa kwa watanzania, mzazi unatakiwa kuwa unamsikiliza mtoto wako
kujua nini anataka na ana matatizo,malengo gani katika maisha yake ya kila siku.
Mtoto
ana haki ya kucheza,
haki hii ya mtoto inamsaidi kuweka mwili wake kuwa imara na wakati mwingine
kufurahi kwa kubadilishana mawazo na wenzake.
Mtoto
ana haki ya kutopigwa na wajibu wakutopiga wengine, kwa kupewa na kufundishwa maadili mema ya kuheshimu wengine wakubwa na wadogo na kuto wakosea kwa makusudi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni