Ni muhimu sana kumuomba Mungu kwa ajili ya watoto
wetu. Lakini hii haiondi jukumu letu katika kuwalea na kuhakikisha wanakuwa na
maisha bora na salama. Mambo mengine yanawatokea watoto sababu ya uzembe wa
wazazi. Inashangaza sana kumuona mzazi anampa ice cream mtoto wa miaka miwili
kushuka chini. Ukimuuliza anasema anapenda, jamani mtoto anawezaje kupenda kitu
asichokijua? Kama hujawahi kumpa atakipendaje? Je kila anacholilia unampa?
Lingine mtoto anafanya anachotaka mzazi yeye anafuata
tu. Akitaka katuni sawa, kucheza tuu muda wote sana, akizira sawa, akilialia
ovyo sawa…yani mtoto ndiye anapanga ratiba yake na ya mzazi. Hapa unamfanya
mtoto kuona kuwa dunia ni kama yeye anavyotaka iwe na hakuna changamoto.
Unamharibu sana sana na matokeo yako hutaweza kumsaidia akishakuwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni