Dondoo hizi zitakusaidia kwa mtoto wa kuanzia miaka
miwili kuweza kujifunza kujitegemea katika mambo mbalimbali:
1. Mtoto anapovuliwa nguo / kuvua ili aende kuoga
muonyeshe wapi pa kuweka nguo chafu na muache awe anafanya hivyo yeye mwenyewe.
2. Kuwe na sehemu maalumu ya kuweka toys za watoto na
mtoto aelewe kuwa kila anapomaliza kuchezea awe anazirudisha mahali pake. Hii
itamjengea tabia ya kupanga vizuri vitu vyake.
3. Kwa wale wa miaka minne na kuendelea unaweza
kununua majagi madogo ya kuweka maji na juisi ili waweze kumimina kwa
ajili yao wanapokuwa mezani, hivi wanakuwa wanajifunza kujitegemea.
4. Wale wanaofundishwa kutumia poti ni vyema
ukimvalisha nguo ambazo ni rahisi yeye kuvua pale anapohitaji poti. Suruali na
kaptula ziwe zenye mpira kiunoni na sio zipu au vifungo maana itakuwa
ngumu kuvua hali itakayompelekea kukata tamaa ya kuendelea kujifunza.
5. Kwa wenye miaka mitatu na kuendelea wanunulie
vyombo imara vya udongo na hii itawafanya wajione sehemu ya familia kuliko kila
mara wao wawe wanatumia plastiki na wakubwa vya udongo. Pia wataona
wanathaminika na watajifunza kujali na kuwa makini maana wanajua wakidondosha
au kutupa kitavunjika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni