Wazazi afya za watoto na ufanisi wao shuleni
unategemea sana malezi yetu na ratiba za nyumbani. Ili mtoto awe na afya njema
na kuweza kumsikiliza mwalimu darasani vizuri na kuelewa ni lazima awe amekula
mlo wenye afya na kulala kwa muda wa kutosha. Ni lazima watoto wale mlo kamili
wenye virutubisho vya kutosha na sio kila siku junk food, juice za mabox na
biskuti. Mzoeze mtoto kula vyakula vyenye afya hasa mboga na matunda na
mtengenezee juice natural na sio za viwandani.
Pia muda wa kula hasa chakula cha usiku ni wa
muhimu sana. Mtoto asile zaidi ya saa mbili usiku yani mbili kamili hivyo muda
wa kula ni saa kumi na mbili na saa moja basi. Na baada ya hapo anacheza au
anafanya homework na saa mbili na nusu hadi tatu ni muda wa kupiga mswaki na
kulala. Mtoto anaenda shule saa kumi na mbili asubuhi, hadi saa nne hajalala
hivi unategemea atamsikiliza mwalimu kweli na unakuta amekula saa tatu usiku.
Mjengee mtoto utaratibu mzuri na utamsaidia sana
maana atakuwa hivyo na ataweza kupangilia muda wake maana kazoezwa kuishi kwa
mipango. Ijumaa na jumamosi anaweza chelewa kulala maana haendi shule kesho
yake ila kula isiwe zaidi ya saa mbili kila siku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni